Tuesday, 21 August 2018

KC GLOVES NA BARAKA DA PRINCE KUDANDIA COLLABO - Bonyeza Star




Mkikuyu Mjaka

Msanii wa miziki aina ya RnB ambaye anaenda kwa jina KC Gloves kutoka Migori ameangukia collabo na star wa Tanzania Baraka da Prince. Akiongea na Bonyeza Star kupitia njia ya simu siku mbili zilizopita  

KC alionyesha furaha yake na kuahidi kuwa atajikaza vilivyo alimradi aiweke county yake ya Migori Kenya kwenye map . KC ambaye anaendelea kuomboleza baada ya kumpoteza baba mzazi wiki iliyopita amesema shuguli hiyo itaendelea wiki chache baada ya mazishi.


 KC Gloves na Baraka da Prince walikutana katika shown moja ya nguvu iliyowaleta pamoja wasanii kutoka Tanzania na wale wa Migori Town pale Gilly Hotel . Kwa sasa wasanii mbalimbali wa Migori wanaendelea kutuma rambirambi9 zao kufuatia msiba huo wa baba KC kuaga dunia .


No comments:

Post a Comment