Saturday 26 November 2016

TANZANIA : SHABIKI WA DIAMOND PLATINUMZ ASEMA OMMY DIMPOZ BADO HATOSHI MBOGA

Ommy Dimpoz & Diamond Platinumz

By Mkikuyu Mjaka



Akiongea kupitia mtandao wa facebook ,shabiki huyu wa Mond  alionekana kugadhabishwa sana na matamshi ya msanii huyo wa Bongo Ommy  Dimpoz ya hapo awali.Hii ni kutokana na majibu ya Diamond kuhusiana na bifu yake na Ommy hivi majuzi  .Hivi ndivyo   Enoch Tipape Lui alivyomwongelea Ommy

"BILA ALI KIBA NA DIAMOND,OMMY DIMPOZ HANGEFIKA ALIPO
Ok leo nimeona kidogo nimuangazie msanii wetu anayeitwa @ommydimpoz kwanza namkumbuka mara ya kwanza naona nyimbo yake ya #NaiNai na @officialalikiba ndo nikajipa nafasi ya kuiangalia zaidi pale nikagundua ok kuna mtu anayeitwa @ommydimpoz lakini baada ya wimbo ule sikuona tena ukaribu na Kiba ghafla nikashangaa bwana Dimpoz yuko karibu na @diamondplatnumz. Ukaribu ule nakuja kuona huyu bwana anapata tuzo ya msanii chipukizi Kili Music Awards nikasema ok baadae nikaona ukaribu wake na Mondi unazidi,ukafikia hatua amekua kama dancer wa Mondi kila show yumo nikaja kumuona @ommydimpoz kwenye show ya Diamond ya 'Are Forever' akapewa kipaza sauti akasema kwa sauti," Namshukuru sana @diamondplatnumz yeye ndo kanifanya leo na mimi napata show,alinishauri nisiogope kutoa nyimbo na kunipa imani kuna siku nitatoboa kwakweli namshukuru sana @diamondplatnumz". Hayo ni maneno aliyosema mbele ya mamia ya watu,nikaamini yeye yuko na mtu mkubwa atakua mkubwa pia,ila mambo yakaenda badae nikaona amebaki kama yeye,akatoa nyimbo zake,akatoa #Wanjera akatoa promo kubwa ila ukweli haikua na impact kubwa sana iliisha kirahisi sana,bwana Ommy akakaa chini akaamua kutoa wimbo mwingine #AchiaBody huu ndo kabisa hata views Youtube ziligoma kabisa wimbo ukaisha bila impact,pia akaachia wimbo ghafla unaitwa #Hawapendagi daah ndo kabisa ukamrudisha dimpoz level za akina @iam_mziwanda yani kiwango cha kawaida sana,ikabidi amekaa kimya mwaka mmoja.,Sasa juzi amekuja na #Kajiandae amefanya na @officialalikiba ,ukubwa wa huu wimbo ni 80% sababu ya uwepo wa Kiba.Je,atakua na Ali Kiba kwa muda gani ili amsaidie kumpa msaada??? Ommy Dimpoz ebu jitathmini kijana,muziki una vijana wana njaa ya mafanikio kama @harmonize_tz @rayvanny @barakatheprince_ sio siri utapotezwa kwenye game soon.Ulimtusi marehemu Ngwea,unamtuhumu Mondi kua ananunua views,anafanya mziki wa ujanja ujanja,we yako ambayo sio ya ujanja umekufikisha wapi? Ila wanasema kama hutowaweza kushindana nao,jiunge nao."
Aliyekuwa mpenzi wa Diamond,Wema Sepetu akiwa na Ommy Dimpoz

No comments:

Post a Comment