Wednesday 12 October 2016

CHRIS BROWN AKATAA OMBI LA MILLARD AYO, CHURCHILL NA WILLY. M. TUVA LA KUTAKA KUMHOJI


Chris Brown


By Mkikuyu Mjaka

Wikendi iliyopita ilikuwa moja ya zile  wikendi bomba kabisa Nchini Kenya Jijini Mombasa ambapo alikuwepo msanii Chris Brown kutoka  Marekani. Msanii huyo ambaye anaimba aina ya muziki wa R&B aliwasili  humu nchini tarehe nane na kuondoka tarehe tisa baada ya kutumbuiza mashabiki wake ambao vilevile  walifurika si  haba  .Ila habari zinazotufikia kwa sasa  ni kwamba msanii huyo alikataa ombi rasmi la wanahabari kutoka pembe zote za Africa kumhoji wala kumchukua video kwa minajili ya kupeperusha  kupitia program mbalimbali .Aidha inaaminika kwamba iwapo mamilioni ya pesa yangeongezwa katika bajeti ya Chris Brown basi angalitenga muda kidogo wa mahojiano.

Millard Ayo,Churchill,Willy M Tuva


Miongoni mwa wanahabari waliowasilisha  ombi lao kwa msimamizi wa msanii huyo ni Millard Ayo wa Millard Ayo Tv  kutoka nchini Tanzania, Churchill  wa Churchill Show pamoja na Willy M Tuva wa Mseto E.A .Kulingana na umaarufu wa muimbaji huyo inasemekana kwamba japo alikuwa na uwezo na hata nafasi ya kufanya ivyo ila mkataba aliokuwa nao na waandalizi wa tamasha hilo,Wale Wasee,haikutilia maanani mahojiano na wanahabari wa humu nchini isipokuwa wale wanahabari rasmi wa Wale wasee. Bonyeza Star pia iliweza kupata maelezo zaidi kuhusiana na msanii wa kike maarufu sana Nicki Minaj kufika Kenya wakati wowote kabla ya mwisho wa mwezi wa Disemba na kulingana na waandalizi huenda akalipwa zaidi ya milioni tisini (90M) alizolipwa Chris Brown 


Nicki Minaj

.Hatuna la ziada ila kuwapongeza wasanii wetu wa Africa Mashariki Ali Kiba,Venessa Mdee ,Nazizi pamoja na Wizkid kutoka Nigeria kwa kazi yao nzuri. Hizi hapa ndizo picha ambazo aliweza kuzichukua Millard Ayo kwa umbali na hata zikaweza kutumika na vyumba vingine vya habari humu nchini .







No comments:

Post a Comment