Tuesday 27 June 2017

RAYVANNY AFICHUA ALIVYOKUMBWA NA UHABA MAISHANI KABLA YA KUKUTANA NAYE MADEE~ Bonyeza Star

Rayvanny

By Mkikuyu Mjaka

- Mwanamuziki wa Tanzania  Rayvanny hivi majuzi alifunguka kuhusu maisha yake ya  awali kabla ya yeye kuwa superstar  na kupata hela.

- Msanii huyo wa Wasafi aliamua kuongea kuhusu maisha yake ya awali baada ya
kushinda tuzo la BET.

- Vanny alimshukuru sana Madee ambaye alisema alimsaidia sana wakati bado alikua fukara kipindi  staa
huyo aliishi na Madee alipokuja Dar kutafuta riziki.



 “Nakumbuka Miaka Sita Iliyopita ndio kipindi Ambacho nilikutana na Unaemuona mbele
yangu.kipindi hicho Sikujua nilicho nacho pia sikujua Wapi nianzie na nini nifanye.Kilikua kipindi kigumu sana Kwangu sababu nilikua Mgeni Dar as salam.Lakini kaka angu @madeeali Alisimama na mimi Kila Alipokua
Akienda Alienda na mimi na hii yote ni baada ya kuniona mnyonge Nisie na msaada.Nilijuana na Wadau na baadhi ya wasanii Kupitia kaka angu @madeeali Pia Alikua  akinipeleka studio na kunishauri Vitu vingi sana vya kimaisha na mziki pia na kusisitiza kua Nisikate tamaa.


Rayvanny and Madee


Rayvanny na Madee “Nimepata Uzoefu Mkubwa wa kutumbuiza mbele  ya kundi la watu kutoka kwake.Kuna kipindi nilikosa hata Nguo zakuvaa Alikua akinipa hata nguo alizokua akizipenda yote kunistiri mdogo wake.Nakumbuka kuna kipindi Akasema mdogo wangu Ray jifunze gari,nikamkatalia na kumwambia kwamba mimi ntaendesha Wapi gari na Ntakuja lini kupata gari.Akaniambia mdogo wangu Una kitu Ambacho kitakusaidia  baadae yote yatawezekana.Alianza kunifundisha Gari yake japo nilikua naigongesha gongesha
kwenye mashimo sababu nilikua sijui lakini Alinivumilia hadi nikajua . Pia Nikawa mjanja wa vitu vingi na kujiamini kisa yeye.Siku Nilipomwambia Naenda Wasafi nilijua hatonielewa Lakini Ndio Alikua mstari Wa mbele mambo yangu yafanikiwe nae Akichangia mpaka #Raymondtiptop Akawa #Rayvanny Hadi leo Hii Tumechukua Tuzo kubwa duniani #BETAwards MUNGU AKUBARIKI KWA MOYO HUO HUO SINA CHA KUKULIPA MUNGU PEKEE NAKUSHUKURU WEWE NA FAMILIA NZIMA YA SENEDA…. HUU MWANZO MUNGU MWEMA 
@madeeali” Rayvanny aliandika.


No comments:

Post a Comment