Thursday 20 July 2017

AG MEDIA HOUSE KUMSAINI LUCIANA-J NA G-TON IKIWA COLLABO NA BARAKA DA PRINCE IPO NJIANI - Bonyeza Star.

Baraka Da Prince


By Mkikuyu Mjaka 

- Baada ya kufanya kazi za msanii Nassizu Murume  na  kuweza kufikisha mbali kijana huyo,  producer wa Nassizu Murume ambae pia ni mmiliki wa AG MEDIA HOUSE ukipenda Angaza  Online Radio & Tv sasa amesaini wasanii wawili  (2) ambao anasimamia kazi zao kwa sasa.

- Akiongea na Bonyeza Star kupitia njia ya simu , Producer Thony Touch amesema h apendi kuona vipaji vikipotea na ndo maana anaamua  kusaidia vijana ambao wanajituma kwenye  muziki na kuwafikisha mbali,

Luciana J


- Miaka miwili zilizopita ( 2015) Thony Touch  aliweza kufanya kazi  na msanii  Lang katalang akiwa amemshirikisha  Chege Chigunda kutoka Tanzania  na kwa sasa anarudi na  renix ya kazi hiyo na wasanii wengine akiwemo Chege Chigunda bado

- Kwa upande mwingine Luciana J yupo kwenye maandalizi ya kufanya ngoma na  msanii mkubwa kutoka Tanzania Baraka De Prince kwa ivo  sasa hivi  tupo kwenye mazungumzo kukamilisha kazi hiyo.

G-Ton



''watu wakae mkao wa kula kwa kazi nzuri za wasanii wadogo mwenye vipaji na muonekano.'' Alimalizia producer huyo

No comments:

Post a Comment